Saturday, 18 June 2016

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA ANDREW KIWHELO ALIVYOWEZA KUSEMA YALIYOMOYONI MWAKE KUHUSIANA NA KITUO CHA RADIO PRAISE POWER RADIO

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Andrew Kiwhelo aliweza kufika katika studio ya Rumafrica na kuweza kusema machache kuhusiana na Redio Praise Power 99.3FM alikuwa na haya ya kusema,
Bwana Yesu apewe sifa watu wa Mungu. Kwa jina naitwa Andrew Kiwhelo mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na mzaliwa wa Iringa ila naishi jijini dar es Salaam, nimeoa mke mzuri na mpenda kutoka nchini Kenya. Leo hii nipo mahali hapa kuelezea jinsi navyoifahamu redio ya Praise Power 99.3FM ambayo iko chini ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar esa salaam Tanzania.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Andrew Kiwhelo (kushoto) na mtangazaji wa Praise Power Radio 99.3FM Ben Bonge na Rumafrica Lets Talk katika studio ya Rumafrica

Binafsi nimeifahamu Praise Power Radio kipindi nipo kwenye bendi moja ya muziki ambayo siwezi kutaja jina kwa sasa. Nakumbuka siku moja katika harakati zetu za kutaka kuzitangaza nyimbo zetu redio, tuliamua kukaa chini na waimbaji wenzangu na kuamua kupeleka nyimbo zetu Praise Power Radio ili zipigwe na kusikika na watu wengina nah ii  ilikuwa ni mwaka 2004 au 2005

Praise Power Radio imefanyika faraja kubwa sana katika maisha yangu na pia kwa Watanzania walio wengi. Mimi kipindi hicho cha nyuma nilikuwa mshiriki wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na nimeona uzuri wa hii redio.

Nimebahatika kusikiliza redio nyingi sana hapa Tanzania lakini Praise Power Radio imekuwa faraja sana kwangu ukifananisha na redio zingine. Redio hii imekuwa haibagui aina ya watumishi wa Mungu. Kwetu sisi waimbaji tumekuwa tukipata ushauri kutoka kwa watangazaji tunapopeleka nyimbo zetu redio, na pale ambapo kuna upungufu wamekuwa wakitushauri cha kufanya ili kuboresha huduma yetu ya uimbaji.

Tunamuomba sana Mungu azidi kumbariki sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maono ya kuanzisha kituo hiki cha redio. Kupitia redio hii mimi nimeweza kufahamika na watu wengi sana kuanzia ile albamu yangu ya kwanza na ile ya pili, hakika wameweza kusimama na mimi tangia kipindi hicho cha nyuma mpaka leo hii. Praise Power redio imenisaidia sana kwa mambo mengi mno ambayo mengine siwezi hata kuyataja.

Ningependa kushauri kwa yeyote ambaye amewahi kusikiliza Praise Power Radio 99.3FM na Yule ambayo nib ado wajitahidi sana kuendelea kusikiliza redio hii kwa kuna vipindi vya kukuelimisha kutoka kwa watangazaji ambayo wamejitoa kufanya kazi ya BWANA na wamejipanga vizuri pia wanajituma kumtumikia Mungu kwa unyeyekevu sana.

Mimi binafsi ninapenda sana vipindi vya Praise Power Radio 99.3FM hasa kipindi cha Rise and Shine chini ya Veronica Frank, Kesha na Praise Power chini ya Erick Brighton na John Kissaka, Sifa Moto chini ya Bony Magupa, Jamvi Chini ya Ben Bonge, Joyce na Frida, pia kipindi cha Power Drive ambacho huzungumzia nchi yetu ya Tanzania kwa undani zaidi, Faraja Time chini ya Victor Aron

Kuna watu wengi sana wanabarikiwa sana na vipindi vya Praise Power Radio, watu wanapokea miujiza yao na uponyaji wanaposikiliza watangazaji na watumishi wa Mungu wanahubiri kupitia redio hii

Watangazaji wamejipanga vizuri na katika mazungumzo yao wanatoa maneno ya faraja kutoka kwenye Biblia. Radio ya Praise Power haichagui rangi, kabila, taifa wala jinsia, ni radio ya watu wote.

Mwisho nataka kuwajulisha kuwa nyimbo zangu unaweza kusikia katika redio hii ya Praise Power Radio 99.3FM na albam yangu mpya ya BUSH TO TOWN inapatikana sokoni kwa sasa. Kwahiyo ukitaka kusikiliza nyimbo zangu kama vile ONEKANA LEO na nyingine nyingi usikose kusikiliza hii redio ambayo ni mkombozi wetu katika kutangaza kazi na huduma zetu.


Ukitaka kunipata mimi na ukatamani kunialika kwenye mkutano, semina, kongamano au tukio lolote la kumtukuza Mungu basi wasiliana name kwa simu hizi, o716 470 104 au 0763 416 382, Mungu akubariki sana na endele kusoma Gazeti Rumafrica Online Magazine, Kusilikiza Praise Power Radio na kuangalia Rumafrica Online TV pamoja na Mlima wa Moto TV. Nakupenda